Tuesday, June 1, 2021

Lukaku Chelsea ndo Basi tena

 


  Inter Milan ya nchini Italia wamesema hawata muuza mshambuliaji wao katika dirisha hili la usajili kutokana na kwamba hawakupanga kumuuza mchezaji huyo.

 Katika jitihada za kukifanya kikosi cha Chelsea kuwa tishio Barani Ulaya Chelsea wamepanga kunoa safu yao ya ushambuliaji kwa kuongeza washambuliaji na Romelu Lukaku ni miongoni mwa mapendekezo ya kocha Thomas Tuchel. Hata hivyo mpango huo  unaonekana kugonga mwamba kwasababu Inter Milan bado wanahitaji huduma ya Mbelgiji huyo aliyechangia kwa kiasi kikubwa timu hiyo kutwaa taji la Seria A msimu uliomalizika.

   Imeripotiwa kuwa Manchester City pia wanamuwinda Mbelgiji huyo.

Ancelotti Apewa Shavu Real Mdrid

 

Carlo Ancelotti
   Klabu ya soka ya Real Madrid leo imemtangaza kocha wao wa zamani Carlo Anceloti  kwa mkataba wa miaka mitatu kuwa kocha wao mpya kwa kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Zinedine Zidane aliyejiuzulu nafasi hiyo mwezi uliopita. 
  Kabla ya kuchukua nafasi hiyo ya kuwanoa wababe hao wa soka la Uhispania Ancelotti alikuwa akiwanoa Everton inayoshiriki ligi kuu ya nchini Uingereza (Premier League).  Hii ni sehemu za jitihada za kutaka kuwarudisha wababe hao kwenye ushindani wa soka barani ulaya kama ilivyozoeleka kwa timu hiyo yenye hadhi kubwa barani Ulaya na ulimwenguni kwote kwa ujumla.

 Carlo Ancelotti aliwahi kuifundisha timu hiyo misimu kadhaa iliyopita huku akiwa na kumbukumbu ya kubeba kombe la Ulaya UEFA mwaka 2014. 

Lukaku Chelsea ndo Basi tena

    Inter Milan ya nchini Italia wamesema hawata muuza mshambuliaji wao katika dirisha hili la usajili kutokana na kwamba hawakupanga kumuuz...