Wednesday, May 26, 2021

Machester United wamepoteza fainali ya Europa dhidi ya Villareal

 Mchezo wa fainali wa ligi ya pili kwa ukubwa na hadhi barani Ulaya Uefa Europa League umemalizika siku ya jana huku ikishuhudiwa Villareal wakiwa mabingwa kwa kushinda penati 11-10 baada ya dakika 120 kumalizika kwa sare ya bao 1-1.

 Goli la Villareal lilifungwa na Gerard Moreno dakika ya 29 na goli la Manchester United lilifungwa na mshambuliaji wao Edinson Cavani mapema kipindi cha pili. 

 Baada ya mchezo kumalizika kwa sare mikwaju ya penalti ndiyo iliyoamua mchezo huo na mlinda mlango wa Machester United David De Gea aliwanyima taji Mashetani wekundu baada ya kukosa mkwaju wake wa penalti.

Lukaku Chelsea ndo Basi tena

    Inter Milan ya nchini Italia wamesema hawata muuza mshambuliaji wao katika dirisha hili la usajili kutokana na kwamba hawakupanga kumuuz...