Inter Milan ya nchini Italia wamesema hawata muuza mshambuliaji wao katika dirisha hili la usajili kutokana na kwamba hawakupanga kumuuza mchezaji huyo.
Katika jitihada za kukifanya kikosi cha Chelsea kuwa tishio Barani Ulaya Chelsea wamepanga kunoa safu yao ya ushambuliaji kwa kuongeza washambuliaji na Romelu Lukaku ni miongoni mwa mapendekezo ya kocha Thomas Tuchel. Hata hivyo mpango huo unaonekana kugonga mwamba kwasababu Inter Milan bado wanahitaji huduma ya Mbelgiji huyo aliyechangia kwa kiasi kikubwa timu hiyo kutwaa taji la Seria A msimu uliomalizika.
Imeripotiwa kuwa Manchester City pia wanamuwinda Mbelgiji huyo.

